Bw. Sebastian Ortiz Alcubierre
Bw. Andrés Ortiz Mendoza
Coat of Arm
Ortiz (Tardienta)
Coat of Arm
Alcubierre (Tardienta)
KAMPUNI YETU

Kampuni ilianzishwa mwaka 1939 na Bw. Ortiz Mendoza huko Villa de Tardienta, Huesca (Uhispania).

Ilianza na biashara ya mbolea aina ya BARRAU na baadaye KAMPUNI YA UMOJA WA KIHISPANIA WA MILIPUKO, wakati huo huo ilikuwa inafanya mchanganyiko wa mboji na mkaa kwa ajili ya kilimo.

Mwaka 1960, Bw. Jose Miguel Ortiz (Mwanzilishi wa kampuni ya Mbolea Ortiz Oses), akiwa anaongoza kampuni, aliendelea kuuza bidhaa hizo pamoja na mbolea nyengine za unga. Katika miaka hiyo, wakulima walikuwa wanaweka katika ardhi mbolea za fosfati, amonia salfeti, potasiamu na naitreti, kila moja peke yake na katika nyakati tafauti.

Kampuni ilikua sana kwa uuzaji wa maelfu ya tani za mbolea huko Aragon, Navarra, Rioja, Soria, Burgos, Lerida,Castellon, na Valencia, vile vile ilipewa kazi na Tasisi ya Taifa ya Ukoloni, ya kuendesha minada kadhaa ya mbolea katika vijiji vya Monegros: San Lorenzo del Flumen, Sodeto, Cubre, Orillena, Montesusin, Valfonda, Frula, n.k.

Kampuni ilibaini kuwa kwa kuweka pamoja mbolea hizi tatu, Nitrojini, Fosforasi na Potasiamu (N.P.K), zinaweza kufanyakazi pamoja na kuzidisha kiwango cha mazao, kwa hivyo ikaamua kutengeneza mbolea za chembechembe zilizokuwa na mchanganyiko wa mbolea tatu hizi, na vile vile iliepuka mrundikano katika maghala na ilisaidia kutayarisha mashamba.

Kwa kutumia chombo cha kuchanganyia zege kilichorekebishwa, alianza majaribio na ikafanikiwa kupata mchanganyiko wa chembechembe katika mbolea za CEN, N.P.K na mbolea za kiwandani za BIOMULL, EKORGANIK na EKOLOGIK. Ilikuwa ni kampuni ya mwanzo ulimwenguni kuweza kutangeneza mbolea za punje punje na vidonge.

Kulifanyika tafiti nyingi, uchunguzi, majaribio na uchanganuzi wa kina kwa kutumia michanganyiko ya mawe yenye fosfato na potasiamu, mbolea ngumu na za maji, viwangu mbali mbali vya tindikali, hali joto, muda wa kuwemo katika mashine, kina cha chombo inapoingizwa mbolea, chembechembe zinazotoka katika chombo hicho, kutengeneza chembechembe kwa kutumia kifaa cha kutengenezea chembechembe, mzunguko wa mashine wakati wa kutengeneza chembechembe hizo, wakati wa kukausha na kuzipoza, shinikizo, aina ya tindikali, unyevunyevu, kiwango cha tindikali (pH), n.k., na ikathibitishwa kwamba, fomyula zile zile zikitengenezwa kwa kutumia njia maalumu na kwa kiwango kidogo zaidi, zinatoa mazao mengi zaidi kuliko aina nyengine: katika mahindi, mpunga, aina za machunwa, mazao ya kitropikal, n.k.

Kulitembelewa viwanda mbali mbali na kufanyika mahojiano kadhaa katika idadi kubwa ya viwanda vya Uhispania na katika sehemu nyengine za Ulaya: Sebatul, Loan, Paris, Melum, Pithiviers, Marsella, Ludwishafen, Krefeld, Maheim, Wiesbade, Martigny.

Katika mchakato huo walitoa ushauri wao Daktari Repert (Uswizi), Travis T. Hignett wa Mamlaka ya Bonde la Tannessee (Marekani), Chemische Werke Albert wa Wiesbaden na wengineo.

Mnamo mwaka 1968, Bw. Jose Miguel Ortiz, alijenga kiwanda cha mbolea za NPK za chembechembe huko Lalueza (Huesca) kilichokuwa na mashine za kuchanganyia, kutengeneza chembechembe, kuingiza amoniako, kukausha na kupoza, kilichokuwa na uwezo wa kuzalisha tani 12 kwa saa moja.

Mwaka 1970 vile vile aliagizwa kujenga kiwanda cha mchanganyiko wa mbolea ya chembechembe na madini huko Barcelona. Kiwanda hicho kilikuwa na mashine za kutengeneza chembechembe, kukaushia, kupozea katika chungio, chenye uwezo wa kuzalisha tani 20 kwa saa moja.

Wakati huo huo, alitoa ushauri kwa Halmashauri ya Jiji la Barcelona katika Matanuri ya Kuchomea takataka na kiwanda cha kuozesha takataka. Vile vile kutoa ushauri kwa viwanda vya mbolea: Felipe Fuster, Aprusa, Aborgan, Abonorga, Adubos Fertilmar n.k.

Mwanzoni mwa mwaka 1960, kwa kubaini kuwa usafirishaji na utengenezaji wa mbolea za chembecheme ulikuwa unaongeza gharama, iliamuliwa kutengeneza mbolea hizo hizo au kwa kutumia fomyula zinazofanana, zote katika hali ya maji maji: Mbolea za CEN, FOLIKOPO; MAXIFRUIT; EKOLOGIK na BIOMULL, lakini kwa kutumia taratibu, vidhibiti na hali nzuri zaidi kuliko zinazotumika katika kutengeneza chembechembe. Katika kuendeleza tafiti, imethibitika ndani ya miaka 50, katika majaribio kadhaa mashambani, katika kilimo cha nafaka, mboga mboga, miti ya matunda, mizeituni, mizabibu n.k. kuwa, kwa kutumia pamoja taratibu maalumu, inazalishwa mbole ambayo, kwa kutumia dozi ndogo, inawezekana kutosha kwa hekta moja.

MAPINDUZI KAMILI KATIKA KILIMO.

Mwanzoni mbolea zilikuwa zinauzwa katika ujazo wa lita 5, baadae lita 1.

Kuanzia miaka 25 iliyopita hadi sasa, mbolea zinauzwa katika chupa ndogo za mililita140 na vijichupa vya mililita 3.

Kuanzia mwaka 2011, mbolea hii pia imeanza kuuzwa katika chupa za lita moja. Chupa moja inaweza kurutubisha hekta 10,000 (kwa ajili ya maeneo makubwa ya Ngano, Mizaituni, Milozi, Mizabibu, Uwele, Aina zote za Shayiri, Alizeti, n.k.).

Zinatengenezwa fomyula aina nyingi za NPK kwa ajili ya vilimo aina tafauti.

Vile vile, kama mtu ataagiza, zinaweza kutengenezwa fomyula maalumu kwa ajili kukinga miti dhidi ya baridi kali, ukame au uvamizi wa virusi, bacteria, kuvu, vimelea, kuharibika kwa miti kutokana na dawa za kuulia wadudu n.k.

Katika tafiti hizi, ulipatikana ushauri wa Madaktari R. Klemm na Holle de Pharma (Ujerumani), watunukiwa wa Zawadi za Nobel S.Ochoa (Uhispania) na F. Jacob (Ufaransa), Daktari Schneider wa Celamerck, Daktari Brian Galloway wa Polisciences, miongoni mwa wengine.

Katika mwaka 1994 ilianzishwa Kampuni ya Berlin Export International Ltd., na kuanzia wakati huo, mbolea zinauzwa kwa kutumia jina hilo.

UTAFITI NA USAMBAZAJI

Kwa muda wa miaka yote hiyo, kampuni yetu imeshiriki katika Makongamano ya Kimataifa juu ya mbolea,biolojia, pamoja na pahali kwengineko: Ann Arbor (Michigan), Raleigh (North Carolina), Lisboa, Reins na Melum (Ufaransa), Roma, Bolonia, Berlin, Venice, Munich, Hamilton (Ontorio) na Nancouver (Canada), Ponta Delgada, Azores, Dresde (Ujerumani), Istambul (Uturuki), Madrid, Barcelona, Seville, Pamplona, Sant Feliu de Guisols (Gerona, n.k.

Vile vile inashiriki na kufanya maonesho sehemu nyingi ulimwenguni: Hannover, Franfurt, Nuremberg (Ujerumani); Ultrech (Uholanzi), Paris, Rennes, Clermont Ferrand, Montpellier, Agen, Lyon, Avignon (Ufaransa), Sydney (Australia), Atlanta, Tulare, Jackson, Fresno, San Antonio (Texas), Georgia (USA), London, Stoneleigt (Uingereza), Wells (Austria), Manzini (Swaziland), Lusaka (Zambia), Santo Domingo (Jamhuri ya Dominikana), Budapest, (Hungary) Abidjan (Ivory Coast), Riyah (Saudi Arabia), Atenas, Tesalónica (Ugiriki) Paraguay, Gaborone (Bostwana), Guayaquil (Ecuador), Windhoek (Namibia), Dakar (Senegal), Luanda (Angola), Verona, Cremona, Cesena (Italia), Antalya (Uturuki), Brussels, Moscú, Poznan (Polland), Lisbon, Santarem (Ureno), Casablanca, Marrakech (Moroko), Kuala Lumpur (Malasia), Manila (Philippines), Hong Kong, Pekín, Shenzhen (China), Bankogk, El Cairo (Misri), Johannesburgo (Afrika ya Kusini), Dar Es Salam (Tanzania), Bulawayo (Zimbabwe), Nairobi (Kenya), Tunisia, Algeria, Monterrey, Guadalajara (Mexico), San José (Costa Rica), Guatemala, San Pedro Sula (Honduras), San Salvador (El Salvador), Panamá, David (Panamá), Santa Fe de Bogotá, Quito, Santiago de Chile, Buenos Aires (Argentina), Santa Cruz (Bolivia), Lima (Peru), Sao Paulo (Brasil), Caracas, Valencia (Venezuela), Tokio, Breno (Jaamhuri ya Checa), Tel Aviv (Israel), Skopje (Macedonia), Teherán (Iran), Baghdad (Iraki),n.k.

MBOLEA ZA CEN NA EKORGANIK

Kampuni ya Berlín Export International Ltd., ikiongoza kwa teknolojia ya hali ya juu na mbolea zake za a la cabeza de la alta tecnología con sus abonos CEN y EKORGANIK, ndiyo ya mwanzo ulimwenguni kutengeneza mbolea za dozi ndogo kabisa, ambazo zimeleta mapinduzi katika sekta ya mbolea.

Kampuni liyoshinda Nyota Mbili za Kimataifa za Dhahabu: Moja juu ya Teknolojia, nyengine ya Ubora wa Viwango pamoja na Tuzo ya Heshima katika Biashara.

Mbolea za CEN na EKORGANIC zimesajiliwa katika nchi kadhaa na zinatumika ulimwenguni kote kwa miaka 50 sasa.

Kampuni vumbuzi na anzilishi ya mbolea maalumu kwa ajili ya mazao yenye kiwango cha juu cha ubora, yakiwa na vitamini zaidi, Asidi ya Amonia, Virutubishi vya kujikinga na kensa n.k. pamoja na uwezo wa kustahamili magonjwa ya mitin na magonjwa ya tauni, mafuriko.

Bila ya kutumia naitreti mashambani, katika mazao na katika mimea na miti.

Ni mbolea zinazofaa kwa kila aina ya kilimo.

Kwa kutumia vichupa 1 mpaka 4 huwekwa mbolea hecta 1.

REKODI YA UZALISHAJI NA VITAMINI KUTOKANA NA MATUMIZI YA MBOLEA YA CEN

- Kilo 10.500 za NGANU kwa Hecta. +690 ppm (sehemu 690 kwa kila milioni moja za Triptofani. +0,13 IU/g za Vitamini A. + 6.4ppm za Vitamini C. +0.04ppm za Vit. B12. Uzito maalumu 82.

- Kilo 11.50 za SHAYIRI kwa Hecta. +0.12 IU/g za Vitamini A. +13.1 ppm za Vitamini C. Uzito maalumu 73.

- Kilo 11.200 za SHAYIRI kwa Hekta. 0.12 UI/g za Vitamini A. +10.3ppm za Vitamini C.

- Kilo 22.000 za MAHINDI kwa Hekta. + 155 ppm. a Triptophan na miligramu/kilo zaVitamini E.

- Kilo 14.500 za MPUNGA kwa Hekta con 2.1 miligramu/kilo za Vitamini A, zaidi ya 400% de Vitamini E, na zaidi ya 4% za protini.

- Kilo 215.000 za NYANYA kwa Hekta na 29% za Vit. A, 3% za Vit. C, 5,6% za Sukari.

- Kilo 145 MACHUNGWA AINA YA CLEMENTINE na 90% za machenza ya Gredi A.

- Kilo 80.000 Machenza kwa Hekta. (80% mazuri na, 19% ya Gredi A) pamoja na 9,8% ya Sukari.

- Kilo 14.000 za ZABIBU ZA MVINYO wenye Kilevi 14º kwa Hekta katika ardhi kame.

- Kilo 44.000 Kg. za ZABIBU ZA MVINYO wenye Kilevi 11.3º kwa Hekta katika ardí ya kumwagilia maji.

- Kilo 88.000 za MBATATA kwa Hekta + 46% za Vitamini A.

- Kilo 415 za ZEITUNI kwa mti mmoja + 37% Uwezo wa Uzalishaji.

- Kilo 18.000 za MTAMA kwa Hekta

- Kilo 28.000 za MAJANI YA KULISHA NGOMBE kwa Hekta. + 20% za protini.

- Kilo 40.100 za VITUNGUU THOUM kwa Hekta Kg. + 170% za Vitamini A + 300% za Vitamina C.

- Kilo 40.000 Kg. Za MAPICHI yenye 13% za Sukari, + 7,34 mg. zaVitamini A na 5,5 mg. Vitamini C.

- Kilo 53.000 za MAPARACHICHI kwa Hekta.

- Kilo 110.000 za KIAZISUKARI kwa Hekta, vyenye 19º za sukari,

- Kilo 66.000 za KAHAWA kwa Hekta

- Kilo 72.000 za Machenza aina ya CLAUSELLINA kwa Hekta.

- Kilo 70.000 za PLAMU GOLDEN PLUS kwa Hektapor. calori 65/70.

- Kilo 200.000 za ZUCCHINI kwa Hekta, zikiwa na 44% ya Vitamini A.

- Kilo 86.000 za MIWA kwa Hekta zikiwa na Tani za ujazo 6,25 za sukari

- Kilo 7.600 za RAPA kwa Hekta.

- Kilo za 105.000 MATUFAHA, yenye Vitamini B12, 5 ppm y Vitamini D, na UI/g. 1.

ONGEZEKO LA VITAMINI:

- VITUNGUU MAJI: Vitamini A + 17%.

- MATANGO: Vitamini A + 147%.

- ESPARAGUS: Vitamini A + 24%, Vitanmini C + 76%.

- SALADI: Vitamini A + 39%. Vitamini C + 15%.

- RANGI KATIKA NYANYA: + 80% na Sukari + 5,6%

- MAHARAGE YA KIJANI: Vitamini , + 9%, Vitamini C: 73.

- MAFUTA: Rto. + 37%, na - 1,5º ya uasidi

- MVINYO: RESVERATROL: 17,5% + 1 grado Brix.

- AINA ZA MACHUNGWA: Vitamini C + 100%, Vitamini A + 50%.

- NDIZI: Vitamini A + 50%, Vitamini C + 500%

- PILIPILI BOGA ZA KIJANI: Vitamini A + 362%, Vitamini C + 27%.

- NJEGERE, DENGU: Vitamini A + 210%, Vitamini C + 100%.

KAMPUNI IMEFANIKIWA KUTUNUKIWA MEDALI ZA DHAHABU, FEDHA NA SHABA KATIKA MIVINYO YENYE HADHI NA MAJINA ASILI

MIVINYO MEUPE NA MEKUNDU YA RIOJA.

ZAWADI YA KWANZA KATIKA KUONJA UBORA WA MAFUTA.

ZAWADI YA KWANZA KATIKA MVINYO WA MONEGROS.

UVUMBUZI WA KILIMWENGU KWA KUTUMIA MBOLEA ZA CEN.

- Mpunga wenye Vitamini A na Vitamini E.

- Mahindi yenye Maíz con Triptophan na Vitamini E.

- Ngano yenye Vitamini A na C.

- Mimea ya nafaka yenye mashuke mengi

- Mihindi yenye kuzaa mabunzi mengi.

CEM – MALISHO YA ZAIDA KWA WANYAMA

Katika miaka ya 70, kulifanyika tafiti bila kuchoka katika chakula cha mifugo kwa aina mbali mbali za wanyama, sehemu wanazoishi, hali za chakula wanachokula, joto, baridi n.k.: Ndama, ng’ombe, kondoo, nguruwe, kuku, wanakondoo, mabatamzinga, samaki n.k.

SKutokana na tafiti hizo, kikagundulika kirutubishi CEM: dawa ya ziada katika hali ya maji maji na kwa kutuma dozi ndogo kwa malisho ya wanyama, iliyotengenezwa kwa kutumia virubishi vya nafaka, kwa kutumia mililita moja kwenye kila lita 200 za maji wanayokunya wanyama.

Hivi sasa, baada ya tafiti endelevu za muda mrefu, imethibitika rekodi za uzalishaji wa nyama, maziwa na mayai, lakini utafiti umekwenda mbali zaidi; sasa inawezekana kuongeza protini, uzito maalumu, kupunguza mafuta na kuongeza vitamini katika nyama, maziwa na mayai.

Vile vile, inawezekana kupunguza kolesteroli katika mayai, nyama na maziwa, miongoni mwa faida nyengine, kama vile kustawisha uwezo wa wanyama kujikinga na kuwa na uwezo mkubwa sana wa kustahamili maradhi.

Na zaidi:

Katika maziwa, ya ongezeko la uzalishaji kwa 23%, kupunguza seli za mwillini kwa 40% na kupunguza kwa kolesteroli kwa 45%.

Maziwa: kupunguza kwa kolesteroli kwa 90%, kuongeza Vitamini A na Omega 3 kwa 15%.

Nyama ya Ndama: kuongeza Vitamini A kwa 40%, kupunguza mafuta kwa 50% na kupunguza kolesteroli kwa 50%.

Nguruwe: Kuongeza protini kwa 25%, kupunguza kolesteroli kwa 55% , na kupunguza kolesteroli kwa 50%.

Nyama ya wanakondoo: kupunguza kolesteroli kwa 50%, kupunguza mafuta kwa 60% na kuongeza protini kwa 70%.

Kuku: kupunguza kolesteroli kwa 50%, kupunguza mafuta kwa 58% na kuongeza protini kwa 22%.

Sungura: Kupunguza kolesteroli kwa 58%, kupunguza mafuta kwa 63%.

Samaki: Kupunguza muda wa kukua, kupunguza idadi ya vifo na matatizo ya virusi, na kuongeza muda wa kuhifadi katika masoko.

CEM, imesajiliwa katika nchi nyingi. Inatengenezwa na BIOAGA, Marekani.

MAGONJWA YA WANYAMA

EKatika miaka yote hii, wakati kampuni inapiga hatua hizo, vile vile ilikuwa inafanya tafiti juu ya magonjwa ya wanyama kama vile: homa ya ndama, homa ya sungura, homa ya kupooza miguu, homa ya mbuzi, homa ya nguruwe, kuharisha kutokana na virusi n.k. na matokeo ni mazuri.

Tunaendelea, kwa mafanikio, kutafiti magonjwa yatokanayo na virusi, kensa, uvimbe, n.k.

Kwa kuwa dhamiri ya kampuni sio kutengeza dawa, baadhi ya fomyula dhidi ya virusi zimetolewa kama hisani na nyingi kati yao ni kwa ajili ya kubadilishana teknolojia na baadhi ya Maabara.

Kampuni ya Berlín Export International, Ltd. Ikiwa na uzoefu mkubwa wa utafiti wa kibiolojia, ilianza na inaendelea kutoa mchango mkubwa katika sayansi, viwanda, kilimo na mifugo, kwa uvumbuzi na mchango wake katika kutoa vibali na uenezaji wa teknolojia

VITA DHIDI YA NJAA

Mojawapo ya vumbuzi muhimu sana za kampuni ni kupata fomula ya kupigana na ukame katika nchi masikini: Nyongeza iliyokolezwa ya chakula.

Tukiwa na kiwango kidogo cha nyenzo ghafi, gharama ambayo ni kuanzia Yuro 5 hadi 20, chupa ndogo 10,000 za ml 140 zinaweza kutengenezwa.

Chupa moja inaweza kutoa nyongeza ya chakula inayoweza kutoa mahitaji ya lishe ya watu 60 kila mwaka.

Sehemu ya fomula hii iliuzwa kwa Maabara ya Ulaya mnamo mwaka wa 1977.


INDEX